Polisi Tanzania

  • Mama ameweka rekodi ya kwanza ndani ya Jeshi la Polisi, akifunga kozi wahitimu 954

    Kwa mara nyingine tena Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuweka rekodi kwenye sekta mbalimbali ambapo chini ya uongozi wake, Chuo cha Taalum ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kimekuwa na idadi kubwa ya wahitimu kwa mara moja, katika historia ya chuo hicho na nchi kwa ujumla. Juni 9, 2025, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifunga kozi ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi ambapo kulikuwa na jumla ya wahitimu 954, kati yao maafisa wakiwa ni 780 na Wakaguzi Wasaidizi wakiwa 174. Idadi hii ni kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1961. Kuhitimu kwao kuna maanisha kuwa wamepanda vyeo, hatua ambayo kwa mara nyingine inathibitisha azma yake ya kuboresha ustawi wa watumishi wa jeshi hilo ili kuwaongezea ari na ufanisi katika kutekeleza jukumu lao la msingi la kulinda raia na mali zao. Mfano mmoja unaothibitisha hili, katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 jumla ya maafisa, wakaguzi na askari 16,896 wamepandishwa vyeo ndani ya Jeshi la Polisi hatua ambayo imeongeza morali ya utendaji kazi na ufanisi. Aidha, katika mwaka ujao wa fedha (2025/26) Mheshimiwa Rais anakusudia kuwapandisha vyeo maafisa, wakaguzi na askari 8,325 wa jeshi hilo. Kupanda vyeo kuna ambatana na nyongeza za mishahara hatua ambayo inawawezesha watumishi hao kumudu gharama za maisha na kufanya shughuli zao za maendeleo. Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia anavyotekeleza kwa vitendo dira ya kujenga Taifa lenye haki

    Haki ni moja ya mahitaji ya msingi kwa kila mwananchi. Akitambua umuhimu huo, Julai 2022 Mheshimiwa Rais SamIA Suluhu Hassan alitangaza kuwa ameunda kamati ya watu watano ikiongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chade ambayo inafanya kazi ya kupitia miundo na utendaji kazi wa taasisi za haki jamii, kuhakikisha kuwa zinawahudumia wananchi kwa uadilifu. Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema mapitio hayo ambayo yameanza na Jeshi la Polisi yatafanyika pia katika taasisi nyingine ikiwemo Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, TAKUKURU, Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya lengo likiwa ni kuleta mabadiliko ya kiutendaji yenye matokeo kwenye vyombo hivyo. Hii si mara ya kwanza kwa Rais kuweka wazi azma yake ya kusimamia haki nchini, kwani itakumbukwa kwa agizo lake kwa Polisi kuhusu wenye kesi ambazo hazina ushahidi waachiwe lilipelekea kuachiwa kwa takribani wananchi 2,000 ambao kesi zao hazikuwa na ushahidi wa maana. “Kabla ya kumpeleka mtu ndani hakikisha umefanya kazi yako vizuri. Una ushahidi wa kutosha ndio unakwenda kumsweka,” alisema Rais Samia akizungumza na maafisa wa Jeshi la Polisi na kueleza kuwa mrundikano mkubwa wa mahabusu ni gharama kwa Serikali kwani inalazimika kuwalisha na kuwapatia huduma za afya, lakini pia ni usumbufu kwa familia. Hatua nyingine kubwa katika masuala ya haki chini ya uongozi wa Rais Samia ni pale mahakama ilipotoa haki kwa wafungwa kupiga kura, baada ya kubatilisha kifungu cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambacho kilikuwa kinapingana na katiba. Aidha, ameendeleza mapambano dhidi ya rushwa akiamini kuwa rushwa inamzuia mwenye haki kupata haki yake na asiyestahili anaipata, akitolea mfano wakati wa uchaguzi ambapo wasio na fedha wanaweza kujikuta hawachaguliwi kwa kushindwa kutoa rushwa. Wakati huo huo, ameendelea kutekeleza ahadi yake ya maridhiano kwa kukutana na kuzungumza na vyama vya siasa akifahamu kuwa haki haiwezi kustawi sehemu isiyo… Read More