Migogoro ya ardhi
-
Miongoni mwa sifa nyingi zinazomtambulisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na uongozi ni USULUHISHI na UPATANISHI. Sifa hizi mbili zimeonekana katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na siasa na kijamii (masuala ya ardhi). Tukiangazia migogoro ya ardhi, katika mwaka 2021/22, asilimia 86 ya migogoro yote ya ardhi iliyopokelewa ilipatiwa ufumbuzi. Miongoni mwa migogoro hiyo ipo iliyoshindikana kwa muda mrefu huku ikigharimu uhai wa baadhi ya wananchi na mali zao na kuleta mifarakano kwenye jamii. Baadhi tu ya migogoro mikubwa aliyoitatua ni pamoja na; Kwanza, ametatua mgogoro wa Bonde la Usangu mkoani Mbeya uliodumu kwa miaka 15 baada ya kumega eneo lenye ukubwa wa hekta 74,000 kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kilimo na ufugaji. Pili, Mgogoro wa Gereza la King’ang’a na Kata ya Kingale juu ya eneo lenye ukubwa wa ekari 7,495.74 mkoani Dodoma ambapo ameamua ekari 3,272.4 zibaki kwa wananchi watumie kwa shughuli za kilimo, mifugo na za kiuchumi na Magereza wachukue zilizobaki. Tatu, aliruhusu kaya 269 zilizokuwa zinaishi kwenye eneo la kilomita za mraba 9.6 ambazo ni sehemu ya Pori la Akiba Swagaswaga kubaki kwenye eneo hilo, na wananchi hao watapatiwa elimu ya uhifadhi. Ili kupunguza migogoro ya ardhi na kuhakikisha haiwi na madhara zaidi Rais Samia ameendelea kuyawezesha mabaraza ya usuluhishi kutoa uamuzi kwa wakati, elimu kwa wananchi inaendelea kutolewa, mamlaka zinaendelea kupima ardhi kwa ajili ya kuanisha matumizi mbalimbali pamoja na kufanya maboresho ya sheria zinazosimamia sekta ya ardhi. Read More