Madarasa Tanzania

  • Mheshimiwa Rais Samia avuka lengo la Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano

    Wanafunzi zaidi ya milioni 1 wakianza kidato cha kwanza kwa pamoja leo Januari 9, 2023, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amevuka lengo la ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambao umetoa nafasi kwa kila mwenye sifa kuanza masomo kwa wakati. Katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26), Serikali ilikuwa imepanga kujenga vyumba vya madarasa 4,040, ambapo kwa mwaka 2022 pekee Serikali imejenga madarasa 8000, ikiwa ni takribani mara mbili ya lengo. Kwa ujumla katika miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Serikali imejenga madarasa 2,3000 katika ngazi zote za elimu, huku ikikarabati yaliyokuwa yamechakaa pamoja na kujenga shule mpya zikiwemo shule maalum za sayansi za wasichana kila mkoa. Kwa miaka miwili ya uongozi wake, Rais Samia ameweka rekodi iliyowezesha wanafunzi wote wanaoanza kidato cha kwanza kufanya hivyo kwa pamoja, hivyo kuondoa utaratibu wa chaguzi za awamu ya pili au zaidi, ambazo hushuhudia wanafunzi wakichelewa kuanza masomo. Mafanikio haya ni utekelezaji wa dira ya Serikali anayoiongoza ambayo inalenga kuboresha elimu nchini na kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayekosa fursa ya masomo kwa uhaba wa madarasa. Read More