Madaktari bingwa

  • Madaktari Wamarekani walioalikwa na Rais kufanya upasuaji bure

    Madaktari bingwa 60 wa mifupa na nyonga kutoka Los Angeles, Marekani wanatarajiwa kuwasili nchi Agosti 10 mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu bure ya upasuaji wa magoti na nyonga katika Hospitali ya Rufaa ya Seliani inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Madaktari hao wanakuja kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na watawasili nchini kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Kilimanjaro (KIA) ambapo wanatarajiwa kufanya upasuaji kwa wagonjwa 200 kwa wiki mbili ambapo walengwa ni wananchi wenye hali ya chini. Kuja kwa madaktari hao ni fursa kwa wananchi wenye changamoto hizo kupata msaada ambapo pengine wasingeweza kumudu gharama hizo kwani gharama za upasuaji huo ni kubwa ambazo hufika hadi TZS milioni 75, lakini zitatolewa bure na wataalamu hao. Mbali na kutoa huduma hiyo, madaktari hao pia watatoa mafunzo kwa madaktari bingwa wa hospitali hiyo kuhusu upasuaji wa magoti, mifupa na nyonga, ili hata watakapoondoka, huduma hizo ziendelee kutolewa kwa viwango vya juu zaidi. Ili kuwezesha hilo, Serikali sikivu chini ya Mheshimiwa Rais imeruhusu vifaa vitakavyotumika kwenye upasuaji, dawa na vitendea kazi vingine viingizwe nchini bila kulipiwa kodi. Read More