Kilimo Kijani
-
Kupitia mpango wa Building a Better Tomorrow (Ujenzi wa Kesho Bora) Serikali imeanzisha mfuko wa dhamana kwa vijana na huduma za mikopo nafuu chini ya Mfuko wa Pembejeo ili kuwavutia kushiriki katika ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imeamua kuanzisha mpango huo kutokana na idadi kubwa ya vijana na wanawake kukosa sifa zinazohitajika na taasisi za fedha wanapoomba mikopo. Zaidi ya theluthi moja (34%) ya Watanzania wakiwa ni vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa, Rais Samia amechukua jukumu la kutatua changamoto zao kwenye kilimo, ili kuongeza tija na kuvutia vijana wengi zaidi, ambapo changamoto zilizotatuliwa ni pamoja na mafunzo, upatikanaji wa ardhi, teknolojia na fedha. Kutokana na mkakati wa Rais Samia wa kufanikisha mapinduzi ya kilimo Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetangaza kuipatia Tanzania mkopo wa TZS bilioni 280 kwa ajili ya sekta ya kilimo ikiwemo umwagiliaji na kujenga kituo cha usafirishaji na usambazaji mbolea. Tangu kuanzishwa kwa mpango wa BBT miezi sita iliyopita, tayari imetenga zaidi eka 600,000 nchi nzima na shughuli ya kusafisha mashamba hayo inaendelea. Read More