Kilimo cha Kisasa

  • Mpango wa Mheshimiwa Rais Samia wa kuvutia vijana kwenye kilimo wavuka lengo

    Serikali kupitia mpango wa Building a Better Tomorrow inakusudia kuzalisha ajira milioni 1 kupitia kilimo hadi ifikapo mwaka 2025, ambapo mwamko wa vijana kujiunga na programu hiyo itakayowawezesha kupatiwa elimu, mashamba, pembejeo na masoko umekuwa mkubwa. Akishiriki mkutano wa chakula na kilimo wa wakuu wa nchi za Afrika nchini Senegal, Rais amesema mpango huo wa kuvutia vijana kwenye kilimo ambacho kitakuwa cha kibiashara Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema hadi Januari 25, 2023 tayari vijana 7,000 wamesajiliwa kujiunga na programu hiyo, kiwango ambacho kimevuka lengo. “Pia tumekuwa tukifanya kazi na benki kwa ajili ya mikopo kwa vijana na wanawake. Tuliweza kupunguza riba kutoka asilimia 15 hadi asilimia tisa,” amesema Rais akibainisha lengo ni kuifanya Tanzania kuwa mfuko wa chakula cha Afrika kupitia nguvu kazi ya vijana ambao ni asilimia 34.5 ya Watanzania wote. #KilimoBiashara Tanzania ya kesho, ni Tanzania ya kilimo cha kisasa kinachofanywa na vijana, na hivi ndivyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anavyowezesha vijana. #MamaYukoKazini pic.twitter.com/psP2HkxlxO — Mama yuko Kazini (@mamayukokazini) January 18, 2023 Kupitia mpango huo vijana watapatiwa elimu ya kufanya kilimo cha kibiashara, mashamba yao yatajengewa miundombinu ya umwagiliaji na ghala la kuhifadhi mazao, watapatiwa teknolojia ya kisasa ya uzalishaji, mitaji, pembejeo za kilimo na kuunganishwa na masoko ya mazao yao. Tayari TZS bilioni 3 ambazo zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha mpango huo zimeanza kutumika kuwawezesha walengwa lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa chakula, malighafi, kuzalisha ajira na kubadili fikra na dhana kuwa kilimo hakilipi. Kwa maelezo zaidi namna ya kushirikia katika programu hiyo bonyeza hapa Read More