India

  • Rais Samia anavyotumia Diplomasi ya Uchumi kuchochea maendeleo nchini

    Tanzania imeendelea kutekeleza sera yake ya Diplomasia ya Uchumi inayolenga kujenga na kuimarisha uhusiano wake wa kimataifa na kujenga mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na taasisi pamoja na mataifa mengine ili kuchochea maendeleo. Historia nyingine imeandika baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kushiriki na kuhutubia katika Mkutano wa 15 wa BRICS (Brazil, Russia, India, China, South Africa) ambalo ni jukwaa la nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi duniani ambapo pato la Taifa la mataifa hayo ni quadrilioni TZS 63.3, ambapo pia kutokana na kupokea wanachama wapya sita, kuanzia Januari 2024 nchi sita kati ya tisa zinazozalisha mafuta zaidi duniani zitakuwa mwanachama wa jukwaa hilo. Kwa kushiriki kwenye mkutano huo, Tanzania itapata manufaa makubwa kiuchumi na kibiashara kwani kunaiwezesha kujenga mahusiano ya kiuchumi na biashara na nchi hizo zenye nguvu hatua inayoweza kufungua fursa mpya au kupanua fursa zilizopo za kuuza bidhaa za Tanzania kwenye masoko ya nchi hizo, na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi. Ni wazi pia kuwa mataifa ya BRICS yamepiga hatua kwenye teknolojia, hivyo Tanzania inaweza kujifunza matumizi bora ya teknolojia katika kurahisisha utoaji huduma na kuchochea maendeleo. China ambayo ni mwanachama wa BRICS ni mshirika mkubwa maendeleo wa Tanzania ambapo kwa miezi saba ya mwaka 2023 imeongoza kwa uwezekaji (Foreign Direct Investment) nchini ikiwekeza mtaji wa zaidi ta TZS trilioni 1.2 ambao pamoja na mambo mengi utazalisha ajira kwa maelfu ya Watanzania. Katika mkutano huo Rais Samia alipata nafasi ya kuzungumza na Rais wa China, Xi Jinping, ikiwa ni mara nyingine kwa viongozi hao kukutana baada ya ziara ya Rais Samia nchini China. Mazungumzo hayo huenda yakaongeza uwezekano wa kufadhili miradi muhimu kama miundombinu, nishati, kilimo, na teknolojia, uwekezaji pamoja ushirikiano wa kiusalama. Katika dunia ya sasa, nchi haiwezi kujitenga kama kisiwa, inailazimu kutoka, kukutana na kushirikiana na mataifa mengine ili kufanikisha masuala mbalimbali… Read More

  • #MiakaMiwiliYaMama na Diplomasia ya Uchumi: Shilingi ya Tanzania kutumika kununua bidhaa nchini India

    Azma ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji inazaa matunda ambapo Tanzania na India zimefikia makubaliano ya kibiashara ambayo yatawezesha wafanyabiashara kutoka pande zote kutumia fedha zao (shilingi na rupia) katika kufanya miamala ya kibiashara. Nafasi hii itarahisisha biashara ambapo India ni moja ya washirika wakubwa wa kibiashara na Tanzania ambapo thamani ya biashara kati ya nchi hizi ni TZS trilioni 10.4 katika mwaka ulioishia Machi 2022. Takwimu zinaonesha kuwa katika mwaka wa kwanza wa Rais Samia, India iliingiza nchini bidhaa zenye thamani ya TZS trilioni 5.3, huku ikipokea bidhaa za TZS trilioni 5.1 kutoka Tanzania. Utaratibu huu mpya si tu utakuza biashara kati ya mataifa haya kufikia lengo la zaidi ya TZS trilioni 13.8 mwaka huu, bali pia utaziwezesha kutunza akiba ya fedha za kigeni ambao sasa hazitahitajika kufanya miamala. Watanzania wanaofanya kazi katika sekta za kilimo na madini watanufaika zaidi kutokana na sekta hizo kuingiza bidhaa zaidi nchini India. Kwa mujibu wa wachumi na wataalamu wa biashara, uamuzi huo pia utaimarisha utabirikaji wa viwango vya ubadilishaji wa fedha za kigeni jambo ambalo ni la muhimu sana katika biashara za kimataifa kwani ina usimamizi wa fedha yake tofauti na awali ilipokuwa ikitumia dola za Marekani. Read More