Dkt. Samia Suluhu Hassan
-
Sekta ya Utalii nchini imeipita dhahabu kwa kuwa ya kwanza katika kuingiza fedha za kigeni nchini, ambapo mapato yake kwa mwaka ulioishia Mei 2025 yamefikia dola za Marekani bilioni 3.92 (TZS trilioni 10.2), ikiwa ni asilimia 55 ya mapato yote ya mauzo ya nje. Kiwango hicho ni ongezeko kutoka dola za Marekani bilioni 3.63 kwa kipindi kama hicho mwaka jana. Ongezeko hilo limeipita dhahabu ambayo imeingiza dola za Marekani bilioni 3.83 (TZS trilioni 9.9), na hivyo kuthibitisha ukuaji madhubuti wa sekta ya utalii na mchango wake katika uchumi wa nchi. Mafanikio haya ni matokeo ya hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akitambua umuhimu wa sekta hii katika uchumi wetu ambayo inachangia asilimia 17.2 katika Pato ghafi la Taifa, inachangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni na kuajiri zaidi ya milioni 3. Moja ya hatua iliyochukuliwa ni Julai 8 mwaka huu ambapo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliruhusu kampuni za utalii kutumia fedha za kigeni katika maeneo mawili muhimu: wakati wa kulipia bidhaa na huduma kwa niaba ya watalii wasiokuwa wakazi, na wakati wa kununua magari maalum ya utalii kutoka kwa wasambazaji wa ndani. Uamuzi huo ulipokelewa kwa furaha na Chama cha Waendeshaji wa Utalii Tanzania (TATO) kikieleza kuwa serikali imedhamiria kukuza sekta hiyo yenye mnyororo mrefu wa thamani na kwamba wataendelea kushirikiana nayo ili kuikuza zaidi sekta hiyo. Read More
-
Kwa mara nyingine tena Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya makubwa na kuweka rekodi katika kuwatumikia wananchi. Rekodi hii mpya ni ya Gawio la Serikali ambapo kwa mwaka 2024/25 (hadi Juni 10, 2025) lilifikia TZS trilioni 1.028, kiwango cha juu zaidi katika historia ya nchi yetu. Gawio hilo ambalo ni ongezeko ya asilimia 34 ikilinganishwa na TZS bilioni 767 zilipokelewa mwaka 2023/24 ni matokeo ya mabadiliko ya Mheshimiwa Rais, chini ya Falsafa ya 4R. Awamu ya Sita imefanya maboresho makubwa ya kisera, kisheria na kikanuni yaliyochagia kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, na hivyo mashirika hayo yakapata faida. Aidha, kutokana na mabadiliko hayo, taasisi zilizotoa gawio hadi tarehe ya kupokea ziliongezeka kwa asilimia 47 toka taasisi 145 mwaka 2024 hadi taasisi 213 mwaka 2025, ikiwa ni kati ya taasisi/mashirika 309 ambayo serikali inamiliki/inaumiliki. Akipokea gawio hilo, Mheshimiwa Rais aliwaeleza viongozi wa mashirika hayo kuwa gawio sio fadhila, bali ni wajibu kutokana na uwekezaji wa serikali. Hata hivyo, amewataka kutoyakamua mashirika ili nao waonekane wametoa gawio, badala yake watoe kwa mujibu wa sheria na kulingana na faida waliyopata. Amesema kuwa lengo lake ni kuona mashirika yanachangia angalau asilimia 10 ya mapato yasiyo ya kodi kwa Serikali, ingawa sheria inataka yachangie asilimia 15. Alitumia wasaa huo kusisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi akisema kuwa “sekta binafsi ni kiungo muhimu katika safari ya mageuzi ya sekta ya umma na kwamba popote uhitaji utakapokuwepo, watashirikiana nao. Read More