Chuo cha Taaluma ya Polisi

  • Mama ameweka rekodi ya kwanza ndani ya Jeshi la Polisi, akifunga kozi wahitimu 954

    Kwa mara nyingine tena Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuweka rekodi kwenye sekta mbalimbali ambapo chini ya uongozi wake, Chuo cha Taalum ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kimekuwa na idadi kubwa ya wahitimu kwa mara moja, katika historia ya chuo hicho na nchi kwa ujumla. Juni 9, 2025, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifunga kozi ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi ambapo kulikuwa na jumla ya wahitimu 954, kati yao maafisa wakiwa ni 780 na Wakaguzi Wasaidizi wakiwa 174. Idadi hii ni kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1961. Kuhitimu kwao kuna maanisha kuwa wamepanda vyeo, hatua ambayo kwa mara nyingine inathibitisha azma yake ya kuboresha ustawi wa watumishi wa jeshi hilo ili kuwaongezea ari na ufanisi katika kutekeleza jukumu lao la msingi la kulinda raia na mali zao. Mfano mmoja unaothibitisha hili, katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 jumla ya maafisa, wakaguzi na askari 16,896 wamepandishwa vyeo ndani ya Jeshi la Polisi hatua ambayo imeongeza morali ya utendaji kazi na ufanisi. Aidha, katika mwaka ujao wa fedha (2025/26) Mheshimiwa Rais anakusudia kuwapandisha vyeo maafisa, wakaguzi na askari 8,325 wa jeshi hilo. Kupanda vyeo kuna ambatana na nyongeza za mishahara hatua ambayo inawawezesha watumishi hao kumudu gharama za maisha na kufanya shughuli zao za maendeleo. Read More