Kilimo

  • Mheshimiwa Rais Samia na mapinduzi katika Sekta ya Kilimo

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema sekta ya kilimo nchini inatarajiwa kukua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 ikilinganisha na ukuaji wa sasa wa takribani asilimia 3.6. Akizungumza kwenye mdahalo wa ‘Food Action Partnership: Investing in Greater Resilience’ nchini Uswisi amesema Tanzania imetengeneza fursa za kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya mfumo wa chakula unaotarajia kuongeza uzalishaji wa chakula, kuimarisha maisha ya watu na kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Katika kudhibiti mfumo endelevu wa chakula nchini, Rais Samia amesema jitihada kadhaa zimefanyika, ikiwemo kuanzisha mradi kwa ajili ya vijana huku wakiendelea kuimarisha ukuaji wa shoroba za kilimo pamoja na kuongeza bajeti ya kilimo mara 4 ukilinganisha na ile iliyopita. Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza miradi na mafunzo mbalimbali ya kilimo kwa vijana ili kuongeza tija kwenye kilimo na kuwezesha vijana kushiriki kwenye uchumi wa Tanzania ambapo lengo ni kuzalisha ajira milioni 1 ifikapo mwaka 2025. Mdahalo huo uliohudhuriwa na zaidi ya viongozi 50 kutoka Afrika, Asia, Ulaya na Marekani mbali na Rais Samia wachangiaji wengine walikuwa Rais Gustavo Petro wa Colombia, Tran Hong Ha, Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam na Alvaro Lario, Rais wa Wakfu wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Roma. Read More

  • Ziara ya Rais Samia nchini China yafungua fursa zaidi za Kahawa ya Tanzania

    Wafanyabiashara wa kahawa kutoka Tanzania wanaolengeka kuuza kahawa katika soko la China wametakiwa kujisajili kupitia Wizara ya Kilimo nchini Tanzania, ili kukidhi vigezo vya kulifikia soko hilo. Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amenukuliwa akisema kuwa mabadiliko hayo yatarahisisha usajili wa kampuni za Tanzania zenye nia ya kuuza kahawa katika soko la China ambapo awali kampuni nyingi zilikuwa zikipata changamoto kufanya usajili katika mtandao wa Mamlaka ya Forodha ya China (GACC). Hatua hii ni mwendelezo wa fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo Tanzania inaendelea kuzipata tangu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara nchini China ambapo akiwa na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping walishuhudia utiaji saini mikataba 15 ya kimkakati inayolenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Hadi sasa kampuni saba zimeshasajiliwa kuingiza kahawa nchini China ikiwa ni pamoja Kilimanjaro Cables (T) Limited, Cotacof Limited, Taylor Winch Tanzania Limited, Dorman (Tanzania) Ltd, Kamal Agro Limited, Redloong Investment Company Limited na Ibero Coffee Trading Company (T) Limited. Uhakika wa soko la kahawa unaweka uhakika ajira na kuzalisha ajira zaidi kupitia mnyororo wa uongezaji thamani kahawa, soko la uhakika kwa wakulima na kuongeza mapato ya Serikali kwa kuuza bidhaa hiyo nje ya nchi. Wakati Tanzania ikilenga kuongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,235 mwaka 2021/2022 hadi tani 72,000 mwaka 2022/2023, wakati huo huo inalenga kuongeza mauzo yake ya kahawa nchini China na mipango inaendelea kwa wafanyabiashara wa Tanzania kushiriki katika Maonesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yanayotarajiwa kufanyika Juni 2023 huko Hunan. Read More

  • Fuata link kutuma maombi kwenye fursa ya mafunzo, ardhi na mitaji kwenye kilimo

    Read More

  • Mheshimiwa Rais Samia Suluhu aidhinisha shilingi bilioni 150 kutumika kwa ajili ya ruzuku ya mbolea

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameidhinisha Shilingi za Kitanzania bilioni 150 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea. Kufuatia hatua hii, wakulima 956,920 katika maeneo mbalimbali nchini wameanza kunufaika na mbolea ya gharama nafuu.   Hatua hii ni sehemu ya malengo ya kisera ya serikali katika kumpunguzia mkulima gharama na kuongeza uzalishaji.   Kilimo kinachangia takribani asilimia 30 ya pato ghafi la Taifa ikiwa na maana kwamba katika kila shilingi mia moja ya pato ghafi la Taifa walau shilingi 30 inachangiwa na kilimo.   Mbali na hatua hii ya kupunguza bei ya mbolea, Mheshimiwa Rais ameendelea kuwa muumini mkubwa wa mageuzi katika kilimo akiongoza serikali katika kasi ya kuhakikisha pembejeo zinapatikana, ardhi inarasimishwa na uhuru wa mkulima kuuza mazao yake kwa bei ifaanyo. Uamuzi mkubwa pia wa kisera na kibajeti kuleta mapinduzi ya kilimo umefanyika katika Bajeti ya Mwaka huu 2022/23 ambapo Mhe. Rais Samia ongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 250 hadi shilingi bilioni 990.   Wanufaika wakubwa katika ruzuku hii ya kwanza ya mbolea ni mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Arusha na Songwe.   #MamaYukoKazini #KaziInaendelea Read More