Mheshimiwa Rais Samia Suluhu aidhinisha shilingi bilioni 150 kutumika kwa ajili ya ruzuku ya mbolea

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameidhinisha Shilingi za Kitanzania bilioni 150 kwa ajili ya ruzuku ya mbolea. Kufuatia hatua hii, wakulima 956,920 katika maeneo mbalimbali nchini wameanza kunufaika na mbolea ya gharama nafuu.

 

Hatua hii ni sehemu ya malengo ya kisera ya serikali katika kumpunguzia mkulima gharama na kuongeza uzalishaji.

 

Kilimo kinachangia takribani asilimia 30 ya pato ghafi la Taifa ikiwa na maana kwamba katika kila shilingi mia moja ya pato ghafi la Taifa walau shilingi 30 inachangiwa na kilimo.

 

Mbali na hatua hii ya kupunguza bei ya mbolea, Mheshimiwa Rais ameendelea kuwa muumini mkubwa wa mageuzi katika kilimo akiongoza serikali katika kasi ya kuhakikisha pembejeo zinapatikana, ardhi inarasimishwa na uhuru wa mkulima kuuza mazao yake kwa bei ifaanyo. Uamuzi mkubwa pia wa kisera na kibajeti kuleta mapinduzi ya kilimo umefanyika katika Bajeti ya Mwaka huu 2022/23 ambapo Mhe. Rais Samia ongeza bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 250 hadi shilingi bilioni 990.

 

Wanufaika wakubwa katika ruzuku hii ya kwanza ya mbolea ni mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Rukwa, Arusha na Songwe.

 

#MamaYukoKazini #KaziInaendelea