Kwa muda sasa kumekuwa na malalamiko kuhusu wananchi kutoridhishwa na utekelezaji wa majukumu ya taasisi zinazosimamia haki jinai nchini kuanzia kwenye ukamataji wa mtuhumiwa, upelelezi, utoaji wa dhamana, uendeshaji wa mashtaka, kesi na eneo ambalo aliyehukumiwa anatumikia kifungu chake.
Kutokana na hali hiyo Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai, iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan inakualika mwananchi na mdau wa haki kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuboresha taasisi hizo.
Kwa maelezo zaidi soma tangazo hili;