July 2025

  • Mheshimiwa Rais Samia atunukiwa tuzo ya Afrika kwa mageuzi makubwa na maendeleo ya kijamii

    Kazi ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwatumikia Watanzania na kuchochea mageuzi kwenye kila sekta inaendelea kutambuliwa ndani na nje ya nchi ambapo leo amepokea Tuzo ya Wanawake 100 wenye Nguvu Afrika (The Power of 100 Africa Women Award) kutoka Access Bank Group. Tuzo hiyo ina malengo makuu matatu ambayo ni kutambua na kusherehekea wanawake wa Kiafrika wanaotoa michango ya mageuzi kwa mataifa na jamii zao, kuhamasisha na kuhimiza kizazi kijacho cha viongozi Wanawake katika bara zima la Afrika na kupaza sauti za Wanawake katika kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii barani Afrika. “Mheshimiwa Raisi, leo hii, tunaungana na Waafrika wote kukukabidhi tuzo hii maalumu […] kama kiongozi wa kuigwa ambaye utawala wake shirikishi, mageuzi ya kiuchumi, na utetezi wa jinsia unaendelea kuinua mamilioni ya watu, siyo tu nchini Tanzania, bali barani Afrika na duniani kwa ujumla,” amesema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Access Bank Group, Protase Ishengoma. Mageuzi ambayo Mheshimiwa Rais ameyafanya nchini yameongeza idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi, yamechochea kuimarika kwa biashara na kuvutia uwekezaji, yameboresha huduma za kijamii (afya, maji, elimu), kuimarisha amani, utulivu na demokrasia nchini, pamoja na kuongeza uwezo wa serikali kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo inaboresha maisha ya wananchi. Read More

  • Tanzania yaongoza Afrika Mashariki kwa kuwa nchi yenye amani zaidi

    Kazi ya Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kulinda amani ya nchi yetu imeendelea kutuletea matunda na heshima ambapo Tanzania imetajwa kuwa nchi yenye amani zaidi Afrika Mashariki kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index ya mwaka 2025. Amani ni msingi wa maendeleo yoyote ambayo jamii au taifa linalenga kuyafikia iwe kiuchumi, kijamii na kisiasa. Tanzania kutajwa miongoni mwa nchi zenye amani zaidi kunaendelea kuitangaza sifa njema kimataifa na hivyo kuifanya kuaminia na kuvutia biashara, uwekezaji na watalii zaidi, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi. Akitoa hotuba ya kuhitimisha shunguli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais alisema nchi pamoja na wananchi wake wapo salama kutokana na kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya dola. Aidha, uimara huo umetokana na serikali kuvipatia vifaa vya kisasa, mafunzo, kuboresha maslahi pamoja na kuajiri watumishi wapya hivyo kuviongezea uwezo wa kutekeleza majukumu yake. Ripoti hiyo ambayo imehusisha nchi 163 duniani imetumia vigezo 23 kupima amani ya nchi ikiwemo ulinzi na usalama wa jamii na kiwango cha migogoro ya kitaifa na kimataifa na matumizi. Tanzania imeshika nafasi ya kwanza ikiwafuatiwa na Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi, Somali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini. Read More

  • MAMA aweka rekodi kubwa nne makusanyo ya kodi kwa mwaka 2024/25

    Mwaka 2024/25 umekuwa mwaka wa rekodi kwenye ukusanyaji wa mapato nchini, ukusanyaji wa mapato wa TZS shilingi 32.26, sawa na ufanisi wa asilimia 103.9, umeiwezesha Serikali ya Awamu ya Sita kuweka rekodi kubwa nne. Rekodi zilizoweka ni kuvuka kwa lengo la mwaka la makusanyo ya kodi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015/16. Rekodi ya pili ni kuvuka lengo la makusanyo ya kila mwezi kwa miezi 12 mfululizo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mwaka 1996. Rekodi ya tatu ni kuongezeka kwa wastani wa makusanyo ya kila mwezi hadi shilingi trilioni 2.69, ambacho ni kiwango cha juu zaidi katika historia ya TRA. Aidha, rekodi ya nne ni kufanikisha makusanyo ya juu zaidi kwa mwezi mmoja ambapo shilingi trilioni 3.58 zilikusanywa Desemba 2024. Matokeo haya yamechangiwa na kazi kubwa iliyofanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Miongoni mwa aliyofanya ni kurekebisha sheria na kanuni 66 pamoja na kufuta au kupunguza kodi, ada na tozo 383 ili kuondoa adha kwa wafanyabiashara. Hatua hizo zimeongeza ushirikiano mzuri kati ya TRA na walipakodi jambo ambalo limeongeza utayari wa wananchi kulipa kodi, kukua kwa shughuli za biashara na uwekezaji, kuimarika kwa ufanisi wa TRA katika kushughulikia masuala ya wateja, hasa kutokana na mamlaka hiyo kuongezewa watumishi. Read More