June 2025

  • Mheshimiwa Rais awaeleza wananchi sababu za kuongezeka kwa Deni la Serikali

    Katika hotuba ya zaidi ya saa tatu kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Suluhu Hassan ametumia zaidi ya dakika nane kuwaeleza wananchi kuhusu Deni la Serikali kufuatia uwepo wa upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu juu ya sababu halisi ya kuongezeka kwa deni hilo kufikia TZS trilioni 107. Katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais amesema moja ya sababu ni kupokewa kwa fedha za mikopo mipya na ya zamani ambayo mikataba yake ilisainiwa wakati wa awamu zilizopita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. “… mkopo unaweza kusainiwa leo lakini fedha husika zikaanza kupokelewa baada maandalizi ya mradi kukamilika na mradi kuanza. Hivyo, ili mkopo huo uingie kwenye deni la serikali ni lazima serikali iwe imepokea fedha hizo,” amesema hayo na kuongeza kuwa Awamu ya Sita imepokea TZS trilioni 11.3 ikiwa mikopo ya awamu zilizopita. Aidha, sababu nyingine ni kuimarika kwa dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Tanzania ambapo kutokana na utofauti wa viwango vya kubadili fedha, deni hilo limeongezeka kwa TZS trilioni 3.9. Licha ya kuwa kwa upande wa dola linabakia kiwango kile kile, lakini linapotajwa kwa shilingi ya Tanzania lazima lionekane limeongezeka kutokana na kushuka thamani kwa shilingi. “Hatua ya kushuka thamani kwa shilingi dhidi ya dola ya Marekani isichukuliwe kama ni hatua hasi, bali ilikuwa ni hatua muhimu ya kukabiliana na mtikisiko wa uchumi wa dunia,” amesisitiza Mheshimiwa Rais. Kwa upande mwingine, ongezeko la Deni la Serikali la Ndani kumetokana na mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo na kulipa madeni ya ndani yaliyoiva. Pia, ongezeko limetokana na serikali kutambua madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii kwa serikali kupitia hati fungani maalum isiyo taslimu yenye thamani ya TZS trilioni 2.6. “Lengo la hatua hizi ni kunusu mifuko ya hifadhi ya jamii, lakini pia wastaafu wetu waliotumikia taifa… Read More

  • Siri nyuma ya gawio la kihistoria la zaidi ya TZS trilioni 1 toka Mashirika ya Umma

    Kwa mara nyingine tena Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya makubwa na kuweka rekodi katika kuwatumikia wananchi. Rekodi hii mpya ni ya Gawio la Serikali ambapo kwa mwaka 2024/25 (hadi Juni 10, 2025) lilifikia TZS trilioni 1.028, kiwango cha juu zaidi katika historia ya nchi yetu. Gawio hilo ambalo ni ongezeko ya asilimia 34 ikilinganishwa na TZS bilioni 767 zilipokelewa mwaka 2023/24 ni matokeo ya mabadiliko ya Mheshimiwa Rais, chini ya Falsafa ya 4R. Awamu ya Sita imefanya maboresho makubwa ya kisera, kisheria na kikanuni yaliyochagia kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, na hivyo mashirika hayo yakapata faida. Aidha, kutokana na mabadiliko hayo, taasisi zilizotoa gawio hadi tarehe ya kupokea ziliongezeka kwa asilimia 47 toka taasisi 145 mwaka 2024 hadi taasisi 213 mwaka 2025, ikiwa ni kati ya taasisi/mashirika 309 ambayo serikali inamiliki/inaumiliki. Akipokea gawio hilo, Mheshimiwa Rais aliwaeleza viongozi wa mashirika hayo kuwa gawio sio fadhila, bali ni wajibu kutokana na uwekezaji wa serikali. Hata hivyo, amewataka kutoyakamua mashirika ili nao waonekane wametoa gawio, badala yake watoe kwa mujibu wa sheria na kulingana na faida waliyopata. Amesema kuwa lengo lake ni kuona mashirika yanachangia angalau asilimia 10 ya mapato yasiyo ya kodi kwa Serikali, ingawa sheria inataka yachangie asilimia 15. Alitumia wasaa huo kusisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kukuza uchumi akisema kuwa “sekta binafsi ni kiungo muhimu katika safari ya mageuzi ya sekta ya umma na kwamba popote uhitaji utakapokuwepo, watashirikiana nao. Read More

  • Mheshimiwa Rais aagiza Polisi kudhibiti viashiria vya uvunjifu wa amani nchini

    Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Polisi kutosubiri amani ivunjwe ndipo wachukue hatua, badala yake wadhibiti viashiria vya uvunjifu wa amani, hasa wakati huu ambapo nchi inajiandaa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025. “Niwatake mjipange vilivyo kuhakikisha mnaendelea kudhibiti viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani. Tusisubiri amani ivunjwe,” amesema Mheshimiwa Rais ambapo yeye kwa dhamana aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ndiye mlinzi namba moja wa amani ya nchi. Akizungumza katika sherehe za kufunga kozi ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, mbali na suala la amani Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo mengine kwa jeshi hilo ili kuimarisha ari na ufanisi katika ulinzi wa raia na mali zao, ikiwemo kuzingatia maadili kwa kila askari kumheshimu mwenzake na kuepuka vitendo visiyokubali kama vile rushwa. Maagizo mengine ni pamoja na kuzingatia haki, na kwamba askari hatakiwi kumwogopa mtu yeyote lakini hatakiwi kumwonea yeyote. Pia, amehimiza mafunzo ya utayari ambayo yanaendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, kuimarisha matumizi ya teknolojia, matahali kusomana kwa mifumo, kudhibiti dawa za kulevya na kujenga uhusiano na ushirikiano mwema na jamii pamoja na vyombo vingine vya dola vya nje ya nchi, hasa katika kudhibiti uhalifu unaovuka mipaka. Aidha, amewataka wahitimu hao kuzingatia viapo vyao vya kazi, kuepuka vitendo vya rushwa na kuwa kielelezo cha mabadiliko chanya na maboresho ya kiutendaji kwenye maeneo yao ya kazi. Read More

  • Mama ameweka rekodi ya kwanza ndani ya Jeshi la Polisi, akifunga kozi wahitimu 954

    Kwa mara nyingine tena Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuweka rekodi kwenye sekta mbalimbali ambapo chini ya uongozi wake, Chuo cha Taalum ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kimekuwa na idadi kubwa ya wahitimu kwa mara moja, katika historia ya chuo hicho na nchi kwa ujumla. Juni 9, 2025, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alifunga kozi ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi ambapo kulikuwa na jumla ya wahitimu 954, kati yao maafisa wakiwa ni 780 na Wakaguzi Wasaidizi wakiwa 174. Idadi hii ni kubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 1961. Kuhitimu kwao kuna maanisha kuwa wamepanda vyeo, hatua ambayo kwa mara nyingine inathibitisha azma yake ya kuboresha ustawi wa watumishi wa jeshi hilo ili kuwaongezea ari na ufanisi katika kutekeleza jukumu lao la msingi la kulinda raia na mali zao. Mfano mmoja unaothibitisha hili, katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 jumla ya maafisa, wakaguzi na askari 16,896 wamepandishwa vyeo ndani ya Jeshi la Polisi hatua ambayo imeongeza morali ya utendaji kazi na ufanisi. Aidha, katika mwaka ujao wa fedha (2025/26) Mheshimiwa Rais anakusudia kuwapandisha vyeo maafisa, wakaguzi na askari 8,325 wa jeshi hilo. Kupanda vyeo kuna ambatana na nyongeza za mishahara hatua ambayo inawawezesha watumishi hao kumudu gharama za maisha na kufanya shughuli zao za maendeleo. Read More

  • Mageuzi ya Rais Samia yaongeza gawio la mashirika ya umma hadi bilioni 900

    Moja ya ‘R’ katika falasafa ya 4R ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inawakilisha’Reforms’ (Mabadiliko) ambapo amelenga kutoa fursa zaidi kwa watu wengi zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache. Matokeo ya mabadiliko hayo kiuchumi tunaendelea kuyashuhudia ambapo mabadiliko yaliyofanywa kwenye uendeshaji wa mashirika ya umma umeongeza gawio linalotolewa kwa Serikali kwa mwaka 2024/25. Gawio hilo limeongeza kwa asilimia 40 toka TZS bilioni 633.3 mwaka 2023/24 hadi zaidi ya TZS bilioni 900 iliyokusanywa hadi sasa ambapo lengo ni kukusanya TZS trilioni 1 kabla ya Juni 10 mwaka huu ambapo gawio hilo litakabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais. Aidha, mabadiliko hayo si tu yameongeza gawio bali pia yameongeza mashirika yanayotoa gawio ambapo kwa mwaka huu ni zaidi ya 200 ikilinganishwa na wastani wa mashirika 146 kuanzia mwaka 2021/22 hadi mwaka 2023/24. Mageuzi yaliyofanywa ikiwemo kuyapa uhuru na kuyawezesha kujiendesha kibiashara yamewezesha mashirika yaliyokuwa yanapata hasara kuanza kupata faida. Mageuzi mengine ni kuunganishwa kwa taasisi 14 na kufutwa kwa taasisi nyingine, kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na ufanisi katika kutathmini bodi za wakurugenzi. Haya ni mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita kwani yanaipunguzia serikali mzigo wa kuhudumia taasisi hizo kwa kuzipa ruzuku, lakini pia kunaleta tija ya kuanzishwa kwa taasisi hizo hasa katika kuwahudumia wananchi na kuchangia katika ukuaji wa uchumi. Read More