January 2024
-
Mwanadiplomasia namba moja wa Tanzania, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaendelea kutekeleza kwa vitendo Diplomasia ya Uchumi ambapo sasa Tanzania inakusudia kuvutia uwekezaji wa dola za Kimarekani bilioni 1 (zaidi ya TZS trilioni 2.5) ndani ya miaka michache ijayo, kutoka uwekezaji wa sasa wenye thamani ya TZS bilioni 6.5 ambao umefanyika katika sekta za kilimo, uzalishaji wa viwandani na ujenzi. Ameeleza hayo akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia na ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wafanyabiashara na wawekezaji wa Indonesia sababu zinazowafanya kwanini Tanzania ni sehemu nzuri zaidi kuwekeza. Kwanza amesema ni amani na utulivu uliyopo nchini na Serikali inayofuata misingi ya demokrasia na utawala bora, pili ni eneo la kimkakati la Tanzania ambayo imepaka na nchi nane na ni lango kwa nchi sita kupitia anga, barabara, reli na maji. Aidha, amesema Tanzania inatoa uhakika wa soko la bidhaa zao kwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni 61, huku pia ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye watu milioni 281.5, Jumuiya ya Mendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu milioni 390 na Eneo Huru la Biashara Afrika (AfFTA) lenye watu bilioni 1.2. Tatu ni Tanzania kuwa na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuridhia sheria na mikataba ya kimataifa inayolinda mitaji na uwekezaji wa kigeni. Nne ni utashi wa kisiasa na nafasi ya Serikali kutambua umuhimu wa sekta binafsi kama injini ya maendeleo ya kiuchumi na kuweka msimamo wa kusaidia biashara na wafanyabiashara kukua. Sababu ya tani ni usimamizi imara wa sera ya fedha na uchumi unaowezesha uchumi kuzidi kukua na kufikia viwango vya kabla ya janga la UVIKO19. Kuthibitisha hilo, ripoti ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) imeitaja Tanzania kama moja ya nchi 20 duniani ambazo uchumi wake utakua kwa kasi zaidi mwaka 2024. Katika ziara yake… Read More
-
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anaendeleza mageuzi chini ya falsafa ya 4R ambapo katika muktadha huo leo Benki Kuu Tanzania (BoT) imetangaza riba elekezi ya asilimia 5.5 ya benki kuu (CBR) kwa benki zote zinazokopa katika benki hiyo ambayo itakatumika kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024 kuanzia leo. Mabadiliko hayo yamefuatia taarifa ya BoT ya Januari 3 mwaka huu ambapo ilitangaza kuanza kutumia mfumo unaotumia riba katika kutekeleza Sera ya Fedha, badala ya mfumo unaotumia ujazi wa fedha, mabadiliko ambayo yanalenga kuongeza ufanisi wa sera ya fedha katika kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha shughuli za kiuchumi. Utofauti wa mfumo wa zamani na wa sasa wa utekelezaji sera ya fedha (hyperlink) Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba amesema kiwango hicho cha riba kimezingatia lengo la kuhakikisha thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni inaendelea kuwa imara na kinaendana na malengo ya kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unabaki ndani ya lengo la asilimia 5 na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia lengo la asilimia 5.5 au zaidi kwa mwaka 2024. Kupitia mfumo mpya, pamoja na mambo mengine BoT inatekeleza majukumu yake kwa kupandisha au kushusha kiwango cha riba kwa mikopo kwenda benki za kibiashara, ili kuongeza au kupunguza fedha kwenye mzunguko, kudhibiti mfumuko wa bei, kuimarisha thamani ya shilingi au kukabiliana na changamoto nyingine ya kiuchumi kwa wakati husika. Mfumo unaotumia riba unatumika katika nchi zote za Afrika Mashariki kama sehemu ya mkakati wa kuwa na sarafu moja na benki kuu moja ya Afrika Mashariki, pia unatumika katika jumuiya nyingine za kiuchumi ambazo Tanzania ni mwanachama. Read More
-
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu imeendelea kuleta mageuzi kwenye miradi ya kimkakati ambapo mradi uliosubiriwa kwa muda mrefu wa magadi soda wenye thamani ya zaidi ya TZS trilioni 1 (USD 400 milioni) katika eneo la Engaruka, wilayani Monduli mkoani Arusha umefufuliwa ambapo Serikali imeanza kuhamasisha wawekezaji kwenye mradi huo. Katika kudhihirisha azma yake ya kuona mradi huo wenye tija kwa wananchi na taifa unaanza kutekelezwa mara moja, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameidhinisha kutolewa kwa zaidi ya TZS bilioni 14 ambazo zitalipwa kwa wananchi takribani 300 ambao watapisha mradi huo. Kwa sasa serikali inatumia zaidi ya TZS bilioni 1 kwa mwaka kuagiza magadi soda toka nje ya nchi kwa ajili ya matumizi ya malighafi hiyo viwandani, hivyo mradi huo utaokoa fedha hizo na kukuza mzunguko wa fedha ndani ya nchi pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja 1,000, kukuza biashara na uchumi wa Taifa na kupunguza gharama za uzalishaji, hivyo kushusha gharama za bidhaa. Hadi sasa wawekezaji zaidi ya 10 kutoka nchi mbalimbali wameonesha utayari wa kuwekeza kwenye mradi huo ambapo pia utaliwezesha Taifa kunufaika na uhawilishaji wa teknolojia, stadi na ujuzi kupitia wananchi watakaopata ajira. Magadi soda hutumika zaidi katika uzalishaji wa vioo, mbolea, rangi (dye), sabuni, nguo, vyakula na vinywaji na dawa, hivyo uwepo wa malighafi hiyo utatochea uanzishwaji wa viwanda vya bidhaa mbalimbali ambazo zitauzwa katika soko la ndani na soko la nje, mathalani katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ambalo Tanzania imeanza kunufaika nalo. Mradi wa magadi soda wa Engaruka ni moja kati ya miradi kumi na saba ya kimkakati ya Serikali iliyo chini ya Shirika la Taifa la Maendeo (NDC), ambao unakadiriwa kuwa na akiba ya magadi soda tani milioni 400.3 ambayo yatachimbwa kwa miaka 150 ijayo. Read More
-
Moja ya falsafa za uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ni Mageuzi (Reforms) ambapo mwaka 2023 yalifanyika makubwa ikiwemo kuanzisha wizara mpya, mageuzi ndani ya wizara, kuanzishwa kwa Tume ya Mipango pamoja na mitaala ya elimu. Mageuzi hayo yanaendelea mwaka 2024 ambapo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuanzia Januari 2024 itaanza kutumia mfumo unaotumia riba katika kutekeleza Sera ya Fedha, badala ya mfumo unaotumia ujazi wa fedha, mabadiliko ambayo yanalenga kuongeza ufanisi wa sera ya fedha katika kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha shughuli za kiuchumi. Awali BoT katika utekelezaji wa Sera ya Fedha (kusimamia uchumi, mfumuko wa bei, mzunguko wa fedha, thamani ya shilingi na ustawi wa sekta ya fedha) ilifanya hivyo kwa kutumia kiwango cha fedha kilichopo mtaani (kwenye mzunguko), ambapo ilipunguza fedha kwenye mzunguko au kuziongeza kutokana na hali ya wakati huo, mfano mfumuko wa bei. Katika mfumo mpya wa kutumia riba, ambayo itafahamika kama Riba ya Benki Kuu (CBR), BoT itatekeleza majukumu yake kwa kupandisha au kushusha kiwango cha riba kwa mikopo kwenda benki za kibiashara, ili kuongeza au kupunguza fedha kwenye mzunguko au kukabiliana na changamoto nyingine ya kiuchumi kwa wakati husika. Kwa kutumia mfumo wa CBR, benki kuu inatekeleza makubaliano ya kutumia mfumo mmoja wa utekelezaji wa sera ya fedha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za kiuchumi ambazo Tanzania ni mwanachama. Mbali na kuhakikisha ukwasi katika uchumi, kukuza uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei, riba hiyo itatumika pia kama kiashiria kimojawapo katika upangaji wa riba zinazotozwa na mabenki na taasisi nyingine za fedha nchini. Hii ikimaanisha kuwa, kadiri riba ya BoT itakavyozidi kuwa ndogo, kutatoa uwezekano mkubwa kwa wananchi kupata mikopo kwa riba nafuu zaidi. Hata hivyo, BoT imesisitiza kuwa riba yake haimaanishi kuweka ukomo katika viwango vya riba zinazotozwa na benki na taasisi nyingine za fedha… Read More