• Rais Samia akutana na viongozi wa Ngorongoro, kuunda Tume mbili

    Jumapili, Desemba mosi, 2024 katika Ikulu ndogo ya Arusha, Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa kisiasa na wa kimila wa jamii ya Kimaasai (Malaigwanani) wanaoishi eneo la Ngorongoro na maeneo ya jirani. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kufuatia kuwepo kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya maamuzi ya Serikali yanayohusu eneo la Ngorongoro. Katika mazungumzo hayo Rais Dkt. Samia amesema ataunda Tume mbili ambapo moja itachunguza na kutoa mapendakezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangalia utekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Rais Dkt. Samia amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Serikali na jamii hiyo huku pia akisisitiza ulazima wa wananchi kushirikishwa ipasavyo katika upangaji na utekelezaji miradi inayopita kwenye maeneo yao. Aidha, Rais Dkt. Samia amesisitiza kuwa Tanzania ni nchi inayojivunia umoja wa kitaifa na yenye Serikali inayowahudumia Watanzania wote. Hivyo, ameitaka Ofisi ya Rais TAMISEMI kushughulikia changamoto zinazojitokeza ikiwemo kukosekana kwa baadhi ya huduma za msingi za kijamii katika eneo la  Ngorongoro.   Read More

  • Rais Samia anavyoacha alama za kipekee katika soka la bongo

    Zaidi ya mashabiki 60,000 walioujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam walilipuka kwa shangwe baada ya mwamuzi kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo dhidi ya Guinea na kuibuka na ushindi wa goli 1-0, ushindi uliomaanisha kuwa Tanzania kwa mara ya nne imefuzu kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 itakayofanyika nchini Morroco Tanzania inafuzu kushiriki michuano hii kwa mara ya nne ikiwa imefanya hivyo mwaka 1981, 2019, 2023 na sasa 2025. Kwa hatua hii Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia ya michezo nchini kwa kuwa Rais ambaye chini ya uongozi wake timu ya Taifa imefanikiwa kufuzu kushiriki mashindano haya makubwa zaidi kwa ngazi ya nchi barani Afrika mara mbili tena mfululizo. Mafanikio haya hayatokei kwa bahati mbaya na ni dhahiri kuwa ni matokeo uongozi thabiti na motisha kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Sote tunafahamu namna ambavyo amekuwa akichochea timu za Taifa na hata vilabu vinavyoshiriki michuano ya kimataifa kupata matokeo chanya kwa kuweka motisha ya goli la Mama. Katika mchezo dhidi ya Ethiopia uliofanyika nchini Congo, Rais Samia alitoa ndege maalum iliyowapeleka wachezaji katika mchezo ule na kuwawezeshea kurejea kwa wakati nchini kujiandaa na mchezo dhidi ya Guinea ambao ndio umeipatia Tanzania tiketi ya kufuzu Afcon 2025. Ushindi dhidi ya Guinea ulichagizwa kwa kiasi kikubwa na nguvu ya mashabiki zaidi ya 60,000 walioujaza uwanja wa Taifa. Nakukumbusha tu mashabiki hawa wote waliingia bure kwani Rais Samia aliwalipia wote viingilio ili tu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Taifa Stars. Habari njema zaidi ni kwamba baada ya Afcon 2025, michuano inayofuata mwaka 2027 Tanzania pia imo ndani kwani kwa mara ya kwanza michuano hii itafanyika katika ardhi ya Afrika Mashariki kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya na Uganda hivyo tayari tuna tiketi ya moja kwa moja. Mashindano haya kuja Afrika Mashariki… Read More

  • Ajira 600,000 zazalishwa nchini ndani ya miezi saba

    Kati ya mwezi Januari hadi Julai 2024 jumla ya ajira 607,475 zimezalishwa nchini ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kufikia lengo la kuzalisha ajira milioni 1.2 kila mwaka. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma. Jitihada za kuhakikisha watanzania wanapata ajira zinaakisi lengo la kuzalisha ajira milioni nane kama ilivyoelezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025. Akizungumzia maeneo ambayo Serikali inayaangazia katika kuzalisha ajira ameeleza kuwa Serikali inatumia balozi zake kutafuta nafasi za kazi kwa watanzania kwenye maeneo yalipo balozi hizo.  Vilevile ametaja njia nyingine kuwa ni kupitia taasisi za elimu, wizara na vyuo vikuu ambako baadhi ya watanzania wanapata ajira nje ya nchi, zikiwamo nafasi za utafiti na fursa kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa. Pia Naibu Waziri Katambi ameeleza kuwa Serikali tayari imeanza kutekeleza mpango maalumu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) ili kubaini ajira zinazotangazwa mtandaoni na kuwafikia watanzania katika kanzidata, pia kuwasaidia kwa mafunzo ili kuhakikisha wanastahili kupata ajira hizo. Read More

  • Mama anaiimarisha TAKUKURU mapambano dhidi ya rushwa nchini.

    Ili kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Serikali imekabidhi magari 88 kwa taasisi hiyo. Magari hayo ambayo yatasambazwa mikoa yote Tanzania yamekabidhiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa  kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi hiyo, hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro. Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa huku mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea. Read More

  • Fursa ya nafasi 9,483 za ajira kwa vijana serikalini

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuongeza nafasi za ajira katika taasisi mbalimbali za Serikali ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.   Read More

  • Watalii wafurika nchini miezi iliyotambuliwa kama ‘low season’ miaka ya nyuma

    Ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu hali ya uchumi kwa Mei 2024 imeonesha kuwa watalii wameendelea kumiminika nchini ambapo miezi ya Machi na Aprili ambayo ilitambulika huko nyuma kwa kuwa na idadi ndogo ya watalii (low season), kwa mwaka 2024 watalii wa kimataifa wameongezeka kwa asilimia 21.9 na asilimia 21.8 mtawalia ikilinganishwa na miezi kama hiyo mwaka jana. Hali hii ambayo ni matokeo ya kuendelea kuimarika kwa sekta ya utalii nchini na duniani inaifanya sekta hiyo kuendelea kuwa chanzo kikubwa cha fedha za kigeni ambapo katika miezi hiyo utalii umeingiza dola za Marekani bilioni 3.58 kwa Machi na dola za Marekani bilioni 5.75 kwa Aprili kutoka dola za Marekani bilioni 2.7 na dola za Marekani bilioni 2.8, mtawaliwa kwa miezi kama hiyo mwaka jana 2023. Mafanikio haya yametokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali pamoja na sekta binafsi ikiwemo kutangaza vivutio vya utalii nje ya nchi, huduma bora kwa wageni wanaofika kutalii nchini pamoja na kuimarisha huduma za usafiri, mathalani sekta ya anga. Ripoti ya BoT inaunga mkono utafiti uliofanywa na Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) kwa robo ya Januari-Machi 2024, ambapo kwa ukuaji unaoendelea sasa wa sekta ya utalii, Tanzania ilishika nafasi ya kwanza Afrika na ya nne duniani kwa ongezeko kubwa la watalii ikilinganishwa na kabla ya UVIKO-19, yaani mwaka 2019. Mafanikio na kuimarika kwa sekta ya utalii, pamoja na sekta nyinginezo kama madini, usafirishaji, kilimo kutaendelea kuchochea ukuaji wa Pato la Taifa kufikia asilimia 5.8 mwaka huu.   Read More

  • EPUKA UPOTOSHAJI: Tanzania haijatoa bahari wala madini yake kwa Korea

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu yupo nchini Korea ambapo amekamilisha ziara rasmi na sasa anaendelea na ziara ya kikazi hadi Juni 6 mwaka huu, ambapo hadi sasa Tanzania imeendelea kunufaika na ziara hiyo kufuatia kusainiwa kwa mkataba, tamko na hati za makubaliano ambazo zitaimarisha uhusiano uliopo na kufungua fursa mpya za ushirikiano kwa manufaa ya wananchi wa pande zote. Kufuatia kusainiwa kwa makubaliano hayo, kumekuwa na upotoshaji mitandaoni ambapo moja ya vyombo vya habari kimeeleza kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini. Balozi wa Tanzania nchini Korea, Togolani Mavura amekanusha habari hiyo akieleza kuwa Tanzania haijasaini mkataba wowote na Korea unaohusu bahari wala madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia, na kwamba katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais ameshuhudia utiwaji saini wa mkataba mmoja wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu. Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa hati za makubaliano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za ushirikiano katika sekta za uchumi wa buluu na madini ya kimkakati pamoja na Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA). Amesisitiza kuwa Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika, kwani inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028). Aidha, ameweka wazi kuwa Tanzania ni moja ya nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinazofaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF. Mkopo ambao Tanzania imeupata, tofauti na ilivyopotoshwa na chomho hicho, ni mkopo wa masharti nafuu na una riba ya asilimia 0.01,… Read More

  • Mama Yuko Kazini: Miradi ya uwekezaji yaongezeka mara mbili robo ya kwanza ya 2024

    Mikakati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kupitia Diplomasia ya Uchumi inazidi kuzaa matunda ambapo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili ongezeko la miradi ya uwekezaji kwa asilimia 111, kutoka miradi 100 Januari hadi Machi 2023 hadi miradi 211 kipindi kama hicho mwaka 2024. Thamani ya uwekezaji huo imeongezeka kwa USD milioni 217.98 (TZS bilioni 566.75) kutoka USD bilioni 1.26 (TZS trilioni 3.26) katika robo ya kwanza ya mwaka 2023 hadi kufikia USD bilioni 1.48 (TZS trilioni 3.85) katika robo ya kwanza ya mwaka 2024. Uwekezaji huu utawanufaisha maelfu ya wananchi ambapo idadi ya ajira imeongezeka kufikia 24,931 katika kipindi tajwa kwa mwaka 2024 kutoka ajira 17,016 zilizosajiliwa mwaka jana, sawa na ongezeko la asilimia 46.5. Mafanikio haya ni matokeo ya hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa chini ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikiwemo kuboresha Sheria ya Uwekezaji ambayo inatoa msamaha wa ushuru wa forodha wa asilimia 75, imepunguza kiwango cha mtaji wa uwekezaji kwa wazawa toka USD 100,000 hadi USD 500,000. Mengine yaliyofanyika ni kuwa na kituo cha pamoja ambacho mwekezaji atapata huduma zote, kuwezesha usajili wa miradi kwa njia ya mtandao, kufuta au kupunguza ada na tozo, kurahisisha utoaji wa leseni pamoja na kufanya mikutano na wafanyabishara nje ya nchi, hasa kupitia ziara za Mheshimiwa Rais na maonesho mbalimbali, ambavyo vimeendelea kuitangaza nchi yetu na kuendelea kuimarika kwa amani na utulivu nchini.   Read More

  • 4R Zinajibu: Tanzania namba moja Uhuru wa Vyombo vya Habari Afrika Mashariki

    Matokeo ya mageuzi ambayo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu anayasimamia kupitia falsafa yake ya 4R yanazidi kuonekana kupitia sekta mbalimbali ambapo utashi wake wa kisiasa umeendelea kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari. Mei 3 ya kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari ambavyo huchukuliwa kuwa ni mhimili wa nne wa dola, vikiwa na kazi ya kuwa daraja kati ya Serikali na wananchi, kulinda maslahi ya wananchi, kuunganisha wananchi na kuchochea maendeleo. Mwaka 2024 yamefanyika maadhimisho ya 31 tangu azimio la Windhoek, na maadhimisho ya nne tangu Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani ambapo uongozi wake umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uhuru na hali ya kiuchumi wa vyombo vya habari. Uthibitisho huo unaonekana kwenye ripoti ya Reporters Without Boarders (RWB) ambayo imeitaja Tanzania kuwa namba moja Afrika Mashariki kwa kulinda uhuru wa vyombo vya habari. Aidha, utafiti huo umeonesha Tanzania imepiga hatua kubwa duniani ikipanda toka nafasi ya 143 mwaka 2023 hadi nafasi ya 97 mwaka huu. Utafiti huo umeangazia mambo mbalimbali yakiwemo misingi ya kisheria, hali ya kiuchumi, hali ya kisiasa, usalama wa wanahabari na dhana ya kijamii na kitamaduni. Haya ni matokeo ya dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia ya kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari ambapo alipoingia madarakani alifungulia magazeti na televisheni za mitandaoni zilizokuwa zimefungiwa, ameunda kamati ambayo imekamilisha kazi ya kuangalia hali ya kiuchumi ya vyombo vya habari pamoja na kuruhusu taasisi za Serikali kupeleka matangazo kwenye vyombo binafsi. Mafanikio haya pia yamechangiwa na mabadiliko ya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari 2016 na baadhi ya Kanuni za Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) 2010, na mikakati ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kutoa elimu sheria za utangazaji na kimtandao hivyo kuviwezesha vyombo vya habari kuzingatia sheria. Mwaka 2022 Mheshimiwa Rais aliweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza wa… Read More

  • #ZiaraYaMamaUturuki ni heshima na fursa kwa Tanzania kidiplomasia, kiuchumi na kijamii

    Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ameanza ziara yake rasmi nchini Uturuki kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mheshimiwa Recep Erdoğan. Ziara hiyo ya kimkakati inatarajiwa kuwa na matokeo chanya kidiplomasia, kiuchumi na kimaendeleo ambapo inafanyika kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 14 (tangu mwaka 2010), na miaka saba tangu ziara ya Rais Erdoğan nchini. Tanzania na Uturuki zina uhusiano wa miaka 61 (tangu mwaka 1963), ambapo Uturuki ilifungua ubalozi wake nchini mwaka 1969, ikaufunga mwaka 1984 na kuufungua tena mwaka 2009, na hivyo kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na uhusiano baina ya mataifa haya. Malengo makuu matatu ya ziara hiyo ya kimkakati ni kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo, kufungua fursa mpya za ushirikiano wa kiuchumi, na kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo. Maeneo hayo yanatarajia yatapewa uzito katika mazungumzo atakayofanya na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais Erdoğan. Nchi hizi zina ushirikiano mkubwa kwenye biashara na uwekezaji ambapo Uturuki ni miongoni mwa nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani imewekeza nchini zaidi ya TZS trilioni 1.3 na kuzalisha ajira zaidi ya 6,700. Kwa upande wa Tanzania, huuza wastani wa bidhaa zenye thamani ya TZS bilioni 41 kila mwaka nchini Uturuki. Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) unaotekelezwa na kampuni ya Uturuki, Yapi Merkez ni kielelezo kikubwa cha ushirikiano baina ya nchi, na ziara hii inatarajiwa kuwa chachu ya kuongeza kasi ya kutekeleza mradi huo utakaobadili maisha na uchumi wa Tanzania. Aidha, Uturuki ni mshirika mkubwa katika kukuza utalii nchini ambapo safari za ndege za moja kwa moja kwenda Dar es Salaam na Kilimanjaro zimerahisisha usafiri wa watalii, sekta ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wetu. Katika kufanikisha lengo la kufungua fursa mpya za ushirikiano, akiwa nchini Uturuki, Mheshimiwa Rais Samia atashiriki jukwaa la uwekezaji pamoja na kuzungumza na kampuni 15 kubwa zaidi nchini humo na kuwashawishi kuja kuwekeza nchini. Mheshimiwa Rais… Read More

1 2 3 15